Charles Garnier

Wajesuiti wafiadini wa Amerika Kaskazini.

Charles Garnier, S.J. (Paris, Ufaransa 25 Mei 1606 – karibu na Collingwood, Ontario, Kanada, 7 Desemba 1649) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1636[1].

Aliuawa na Wairoki, kabila lingine la Waindio wakati wa kubatiza wakatekumeni[2][3].

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930.

Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92011
  2. Gray, Charlotte; Angel, Sara (2004). The Museum Called Canada: 25 Rooms of Wonder. Random House Canada. ISBN 978-0-679-31220-8.
  3. Larivière, Florian (1957). La Vie ardente de Saint Charles Garnier. Montreal: Bellarmin.
  4. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy